Google PlusRSS FeedEmail

STEVEN KANUMBA AWAOMBA WASANII KWA FILAMU KWA UJUMLA WAO WAPENDANE

Steven Kanumba, msanii wa Filamu Nchini Amewataka wasanii kuwa na upendo na ushirikiano ili kufika mbali tofauti na ilivyo sasa ambapo msanii ana mambo yake.Alisema wazidi kuzidisha upendo na kusaidiana ili waweze kupiga hatua, kubwa na kufikia kwenye mafanikio kama aliyokuwa nayo yeye na Ray ambapo mpaka sasa ndio wasanii wa kiume wanaolipwa zaidi kwa kuigiza Filamu za Kibongo.Ndani ya hafla ya kutoa tuzo za Mini Ziff aling'ara kwenye ukumbi wa New Maisha Club, Msanii huyo alijinyakulia tuzo mbili kwa mpigo, ile ya Msanii Bora wa Filamu pamoja na filamu yake ya Devil's Kingdom kuibuka kidedea kwa upande wa Filamu yenye Sauti Bora...Pia alitoa wito kwa  jamii inunue filamu za nyumbani ambazo zinauzwa kihalali badala ya kung'ang'ania zile feki zilizozagaa mitaani.kwa maana kama watanunu filamu halali ina maana wao kama wasanii watapata mafanikio na selikali itapata kodi kutokana na mauzo ya filamu hizo..Wasanii wengine waliojinyakulia tuzo ni pamoja na JB ambaye filamu yake ya Senior Bachelor iliibuka Filamu Bora, Cloud alijinyakulia tuzo ya Mwongozaji Bora wa filamu, wakati tuzo ya Msambazaji Bora wa filamu za Tanzania ilikwenda kwa kampuni ya Steps Entertainment.Kwa sasa kanumba yuko mikoani kwa ajili ya kufanya promosheni ya kazi zake.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging