Mwanamuziki aliyeibukia kwenye shindano la Bongo Star Search, Baby Madaha, amejiunga rasmi kwenye Kundi la TMK Wanaume Halisi ambalo linaongozwa na Juma Kassim Ally Kiroboro ‘Sir Nature’.Habari kuwa Baby ni memba wa Halisi, zimethibitishwa na yeye mwenyewe pamoja na kiongozi wa kundi hilo Juma Nature a.k.a Msitu wa Vina.Staa huyo alipoulizwa alikiri kufanya kazi na Halisi na kuongeza kwamba mwaka huu ameamua kujipanga vyema zaidi ndiyo maana ameungana na vichwa vya kiumeni.Kwa upande wa Nature, alijibu: “Unauliza maembe kibada? Baby Madaha ndiye first lady wa Halisi. Tumemchukua kwa sababu anaweza kazi.”aada ya kumaliza msimu wa BSS, Baby alifanya kazi mbalimbali ndani na nje ya nchi lakini alipotoa ngoma yake inayokwenda kwa jina la Amore, ilimtambulisha vema.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.