Kundi la Cash Money,linazidi kujiozolea wasanii nchini marekani,mara baada Christina Milian & Busta Rymes kutangazwa kujiunga na Young Cash Money,kuna habari kuwa,Rapper Lil Wyne akiwa katika mahojiano na kituo kimoja cha radio Nchini Marekani, amekubali kwamba mda wowote kuanzia sasa mwanamama Ashanti atajiunga na kundi lao.Ashanti ambaye ni mwanachama wa kuni la Murder Inc anatarajiwa kusaini mkataba wa kujiunga na kundi hilo Lil Wyne akisikika akisema “sitaki kuvuka mipaka yangu lakini nadhani tunafanya kazi na Ashanti sasa hivi”Mwaka jana Ashanti alifungua lebo yake inaitwa “Written Entertainment” ambayo kwa sasa ina dil na kuipromote single yake ya “The Woman You Love” aliyomshirikisha Busta Rymes wa Cash Money.Ashanti alianza kushine wakati huo wa single kama za Wat’s love na Always on time akiwa na Ja Rule ambapo sasa hawapo tena kwenye lebo moja na wala hawashirikiani kama zamani, nakumbuka siku kadhaa zilizopita kabla Ja Rule hajaenda Jela, alitweet kwamba “nimejaribu kumwambia Ashanti tuungane kama zamani amekataa, ila simlaumu kwa sababu ni dada yangu na ninamuheshimu”
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.