Nyota wa filamu kutoka Maisha Plus Steven Sandhu ambaye kwa sasa anafanya vizuri katika tasnia ya filamu swahiliwood amewaasa wasanii wa filamu kujiendeleza kimasomo zaidi ili kukabiliana na changamoto wanazoweza kukutana nazo iwapo wanaweza kufanikiwa kwenda kuigiza sehemu nyingine tofauti na Tanzania , amesema kuwa awali alikuwa akihofia kuhusu uwezo wa wasanii waliopo katika tasnia ya filamu lakini kwa sasa hana hofu tena“Wasanii wengi tutnahitaji kujiendeleza zaidi kutoka na hali ya utandanda wazi unaotukabiri, awali kabla ya kuingia katika uigizaji nilijua kuwa wasanii wengi wanataaluma katika fani hiyo lakini ukweli ni kwamba wengi wao wanatumia sana vipaji kuliko taaluma, nahisi hali hiyo inaweza kuwa ni tatizo kwa sababu msanii akikutana na msanii wa kimataifa wanaweza kushindwa kufanya kitu kwa pamoja,”anasema Steve.Msanii huyo amekuwa kivutio katika filamu nyingi kutokana na staili yake ya nywele ambavyo uziweka, mwenyewe anasema kuwa awali aliingia katika uigizaji lakini hakupewa mbinu za uigizaji na alikuwa anajiona kama yupo sawa lakini alipobahatika kukutana na Muongozaji wa filamu wa kimataifa Karabani na kufundishwa wakati akiigiza filamu ya CPU alijiona kuwa kumbe alikuwa bado katika uigizaji, anaamini kuwa hali hiyo ndio ipo kwa wasanii wengi nchini.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.