Google PlusRSS FeedEmail

JE KAJALA ATAFANYA VYEMA SOKONI MWAKA HUU?

Nyota anayetesa katika tasnia ya filamu kwa sasa katika tasnia ya filamu Bongo Kajala Masanja ni moja kati ya wasanii wa filamu waliofanikiwa kuingia katika fani ya uigizaji na kuwa wasanii maarufu bila kupitia katika vikundi vya sanaa za maigizo kama ambavyo nyota wengi wamefanya na kuwa wasanii mahiri, lakini kwa binti huyo hali iko tofauti, yeye toka siku aliyoanza kuigiza ni mtu wa kula shavu tu.
“Kwangu ni faraja kwa kuingia katika game bila kupitia katika vikundi vya sanaa na kukubalika, maana wasanii wengi historia inaonyesha kuwa walianza katika vikundi na kisha kuja kuigiza katika filamu, lakini kwangu haikuwa hivyo ni bahati si rahisi kufanikiwa kwa kutoka msanii chipukizi hadi kuwa Star,”anasema Kajala Kajala kwa mwezi huu wa February tunaweza kusema ni mwezi wake kwani ndiye msanii ambaye ameshiriki filamu zaidi ya nne zilizoingia na zinazotegemea kuingia sokoni kwa mwezi huu wa pili na filamu hizo zimetengenezwa na kampuni tofauti tofauti, hivyo inaonyesha msanii huyo alivyo almasi katika tasnia ya filamu kwa sasa.Filamu hizo ni pamoja na filamu ya Kijiji cha tambua Haki kutoka Kanumba the Great Film, filamu ya Shortcut kutoka RJ Company, filamu ya House Girl & Boy na filamu ya Jeraha la Moyo ya Issa Mussa ‘Cloud 112′ ndio maana tunasema kuwa mwezi huu ni wa Kajala sokoni kwani ana filamu nyingi hali ambayo inaonyesha yeye kukubalika katika tasnia hii ya filamu kwa hapa Bongo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging