Google PlusRSS FeedEmail

MARA BAADA YA KUSHINDA GRAMMY CHRIS BROWN ANYOOSHEWA KIDOLE

Mshindi wa Tunzo ya Grammy alioupata wiki iliyopita umefanya jina la Chris Brown lipambe vyombo vya habari duniani kote, lakini wengi wakiupinga. Hata mastaa kama Miranda Lambert na Jack Osbourne waliandika katika mtandao wa twitter kuelezea mshangao wao juu ya ushindi wa kijana huyo. Kilichowafanya wengi wapinge ushindi huo siyo kuwa hajui kuimba, bali ni tukio alilofanya miaka miwili iliyopita la kumpiga na kumuumiza vibaya aliyekuwa mpenzi wake, Rihanna huku tuzo zikiendelea kutolewa ukumbini. Hata hivyo, Brown amewatolea maneno makali wote wanaopinga ushindi wake, huku akijitetea kuwa kila mtu anastahili kupewa nafasi ya pili anapokosea.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging