Google PlusRSS FeedEmail

ODAMA AFUNGUA KAMPUNI YAKE YA FILAMU

Nguli katika tasnia ya filamu Jenifer Kyaka ‘Odama’ ameingia katika kundi la akina dada wajasiriamali baada ya kuamua kufungua kampuni yake ya utengenezaji wa filamu kwa ajili ya utayarishaji wa filamu zake baada ya kutumia kampuni za wadau wengine wa filamu toka kuanza kutengeneza kazi zake binafsi kutoka kushiriki kwa watayarishaji wengine, kampuni yake ambayo ameipatia jina la J. Production itajihusisha na utayarishaji wa muswada upigaji wa picha za filamu ikiwa ni kazi zake na watayarishaji watakaohitaji huduma hiyo“Kwa sasa hali ya ushindani ni kubwa sana kwa hiyo kama hauna kampuni kwa ajili ya utayarishaji wa filamu zako utasumbuka hata kuharibu kazi yako, unapotumia kampuni ya nje unakutana na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kucheleweshewa kazi zako lakini pia unakosa usimamizi wa kazi hiyo, unaweza kupoteza muda kwani unapompatia kazi mtendaji hata kama ana kazi nyingi hasemi, hali ambayo uharibu ratiba kwa kucheleweshewa kazi hata kuharibiwa,”anasema Odama.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging