Google PlusRSS FeedEmail

CHOKI AJITOA TUNZO ZA BASATA KILI MUSIC AWARDS

Mkurugeni na Mwanamuziki wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki ametangaza kujitoa katika shindano la kuwania Tuzo ya Kill Music kwa kile alichodai haoni faida ya kushiriki.Choki alisema kujitoa kwakwe kunatokana na ushiriki wake kila mwaka bila kupata chochote, hivyo haoni haja ya kuendelea kuwa ndani ya shindano hilo kwani limejaa ubabaishaji.
“Tuzo hizi sizipendi kwa sababu siyo za kweli, kila mwaka huwa nashiriki lakini sijaona faida yake, nawaomba Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wazitoe nyimbo zangu zote kwenye shindano hilo,” alisema Choki.
Choki anaungana na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abdul Sykes a.k.a Dully Sykes,ambaye naye alijitoa Wengine ni Tid, hivi karibuni kwa madai kuwa tuzo hizo ni za uongo na hazina maana yoyote kwake..

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging