Google PlusRSS FeedEmail

FILAMU YA SHEMEJI KUTOLEWA ZAWADI KWA WAPENDANAO

Kampuni ya Shark’s Video Production ya jijini Dar es Salaam, imesema kuwa imeingia kwenye tasnia ya filamu kwa ajili ya kuijenga zaidi tasnia hiyo. Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Robert Mhangwa, aliyasema hayo alipokuwa anazungumzia ujio wa filamu ya kwanza ya kampuni hiyo, iitwayo Shemeji.
Filamu hiyo iliyowashirisha wasanii wengi mahiri wakongwe na chipukizi, inatarajiwa kuingia sokoni wiki hii.
Mhangwa alisema kabla ya kuchukua uamuzi wa kuwekeza kwenye tasnia ya filamu, kwanza walifanya utafiti wa kina juuu ya matatizo yanayoifanya tasnia hiyo ishindwe kupiga hatua zaidi“Tumegundua matatizo mengi, kwa hiyo tumekuja kwa lengo ya kuyafanyia kazi matatizo hayo na kuiwezesha tasnia hiyo izidi kupiga hatua zaidi,” alisema Mhangwa.Alisema katika harakati ya kutimiza azma yao, wameibuka na filamu ya Shemeji ambayo anasema kuwa wanaitoa kama zawadi ya mwaka mpya kwa wadau wa filamu za kitanzania..“Filamu hii ya Shemeji tunaitoa kama zawadi tu kwa wapenzi, lakini kuna mambo makubwa zaidi yanakuja. Tumedhamiria kufanya kitu kikubwa katika tasnia hii,” alisema Mhangwa.Aidha amewataka wapenzi wa filamu kuhakikisha wanapata nakala halisi ya filamu hiyo ili waweze kupata burudani na ujumbe mzito uliomo ndani ya filamu hiyo.Wasanii walioshiriki katika filamuj hiyo ya Shemeji ni Hashimu Kambi, Mshindo Jumanne ‘Papa Mkubwa”, Salma Salmini ‘Sandra’, Ibrahim Mbwana ‘Bad Boy’, Ramadhani Mussa ‘Kishoka’. Fadhili Msisiri “Mzee Msisiri’, Rehema Juma na Rashid Altwan.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging