Google PlusRSS FeedEmail

WEMA AZIDI KUWATISHA MASHOST ZAKE...

Wema adaiwa kumiliki bastola, mashosti zake wamuogopa..
Nyeti nzito kwamba Wema Isaac Sepetu anadaiwa kumiliki bastola, zimezua balaa kwa mastaa hivyo kumuogopa kama ukoma wakihofia usalama wao Kwa mujibu wa chanzo makini, mlimbwende huyo aliyekuwa Uarabuni kimatanuzi hivi karibuni, amewafunga midomo mastaa wa kike Bongo wanaopenda bifu naye kwani kwa sasa wanamgwaya baada ya kusambaa kwa habari kuwa ana kifaa hicho.
“Kwa taarifa yenu, mkiendelea kumchezea Wema itakula kwenu, sasa hivi ana mguu wa kuku (bastola), kajiimarisha vilivyo kiulinzi, labda ni kwa sababu anakaa mwenyewe ‘so’ inamsaidia kujilinda,” kisema chanzo hicho.
UTATA ULIPOANZA
Mara baada ya kunyaka taarifa hizo, ripota wetu aliingia mzigoni ili kujua kama kweli staa huyo mkali wa filamu ana bastola, ni kwa nini aamue kujiwekea ulinzi kiasi hicho na je, atakuwa anaimiliki kihalali au la?
UTATA WAANZA KUTATULIWA
Katika nusanusa ya ripota wetu kunako ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa BBM, Wema alitundika picha ya bastola hiyo ikiwa juu ya sakafu ya marumaru inayorandana kwa asilimia zote na ile ya nyumbani kwake, Mwananyamala jijini Dar es Salaam.Dakika chache baada ya tukio hilo, ukurasa huo ulijaa maoni ya mashabiki na mastaa wenzake waliotaka kujua ukweli juu ya bastola hiyo.
Hata hivyo, Wema ambaye muda wote alikuwa hewani hakuwajibu chochote.
HOFU YA ZIDI KUTANDA
Staa mmoja mkubwa aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa tangu Wema arudi kutoka Uarabuni, mastaa wenzake wamekoma kumchokoza kwani tayari wamezipata habari kuwa ana ‘mzigo’ huo.
WEMA ANASEMAJE?
Ili kumaliza utata huo, ripota wetu alimvutia Wema waya na kumtaka kuweka mambo sawa ambapo mahojiano yalikuwa hivi;
Swali: Wema kuna taarifa kuwa unamiliki bastola ambayo hivi karibuni ulitundika picha yake katika mtandano wa BBM, vipi ni ya kwako?
Wema: Ndiyo, ni ya kwangu.
Swali: Duh, kuna taarifa kuwa hata mashosti zako wanakuogopa kwa sasa, unaimiliki kihalali au?
Wema: Hivi ulisema wewe nani…aaah…mmmh… kwanza sikia, siwezi kusema moja kwa moja kama ninayo au sina?
Swali: Sasa mbona unatuchanganya wakati umesema ni ya kwako, kisha tena huwezi kusema moja kwa moja, kuna nini nyuma yake?
Ghafla Wema alikata simu na kila alipopigiwa hakupokea hivyo jitihada za kuichimba habari hiyo zinaendelea.


KWA HISANI YA DEIWAKA

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging