Rihanna amelipa kiasi cha Paundi 15 elfu kwa ajili ya tiketi ya ndege daraja la kwanza kumsafirisha mtengenezaji wake wa nywele baada ya kutoridhika na kutengenezwa na mtu mwingine.Mwanamuziki huyo ambaye sasa yupo Uingereza ambapo yupo nchini humo kwa ajili ya kupiga picha za shoo ya Jonathan Ross,alikwenda kwenye bwawa la kuogelea na baadae katika chumba cha joto ndipo alipogundua kuwa nywele zake hazipo sawa.Akajaribu kuweka vipodozi vingi lakini ilishindikana kurudi kwenye hali yake ya kawaida ndipo alipoamua kununua tiketi ya ndege kwa paundi 15 elfu ili kumwezesha mtengenezaji wake huyo amfuate nchini humo kwa ajili ya kuweka nywele zake sawa.kipindi akiwa anamsubiri mtenegenezaji huyo mda wote wa mazoezi alionekana akiwa amevaa kofia kutokana na kasoro hizo ambazo hakutaka paparaz waone.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.