Google PlusRSS FeedEmail

SOKO LA FILAMU NCHINI LATINGISHIKA

HALI si shwari Swahiliwood katika maduka yote yanayouza filamu za Kitanzania Jana  tarehe 05/03/2012, asubuhi mida ya saa tano baadhi ya wasambazaji walikuwa vikao vya dharura baada ya filamu kama tatu kuingia sokoni huku kila mmoja akitegemea filamu hizo kuuzwa katika bei mpya ambayo hivi karibuni wasambazaji walikutana na kupanga bei hiyo Bei mpya iliyopangwa Tshs. 2,500/= lakini leo filamu zimeuzwa chini ya bei hiyo, bei inayolalamikiwa ni kuwa baadhi ya filamu zimeuzwa kwa bei ya Tshs. 1,500/= hadi 1,250/= kinyume na makubaliano yaliyofikiwa katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa vijana Kinondoni na kutolewa muafaka kuwa lazima filamu zipande bei.
Sababu kubwa ya kupanda kwa bei ya filamu kutokana na uhaba wa malighafi kukosena sokoni na zilizopo kupanda juu sana na kufanya biashara kuwa ngumu kuliko awali, hata hivyo lawama zimemshukia mwenyekiti wa Chama cha wasambazaji Emanuel Myamba ‘Pastor Myamba’ kwa kuonekana msaliti kwa kuingiza filamu yake ya Tears Forever kwa bei ya chini kinyume na makubaliano.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging