Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, ametangaza kiurudi vitani na menejimenti ya Clouds FM.Uamuzi huo, Sugu ameutangaza leo baada ya kutolewa kwa hati ya wito wa mahakamani kwenda kwa wasanii wanaounda Kundi la Mapacha, James Kasulwa ‘Kulwa’ na Levinson Kasulwa ‘Dotto’ ambao ni memba wa mtandao wa Vinega Shauri hilo la mahakamani, Mapacha ni wadaiwa, wakati mlalamikaji ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa Clouds FM, Joseph Kusaga.
Kutokana na wito huo wa mahakama, Sugu amesema kuwa Clouds wamekiuka makubaliano yote ya msingi ambayo yeye alisaini na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM, Ruge Mutahaba, yaliyohusu kumaliza mvutano wa pande mbili.Kwa muda mrefu, Sugu pamoja na Vinega, walikuwa kwenye mashambulizi makali, wakiituhumu Clouds kuua muziki wa kizazi kipya, kudhulumu wasanii na tuhumu nyingine nyingi.Baada ya kupata taarifa kwamba Mapacha wametakiwa kwenda mahakamani Machi 21, 2012, Sugu ameandika taarifa yake kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Facebook: “
TAARIFA YA MASIKITIKO:WALIKUJA NA KUOMBA MUAFAKA NASI TUKAKUBALI KWA AJILI YA AMANI NA MAENDELEO YA SANAA,NAMI KAMA KINEGA MWANDAMIZI NA PIA KIONGOZI(MBUNGE) NIKACHUKUA MAAMUZI MAGUMU YALIYOLETA MACHUNGU YA LAWAMA TOKA KWA MASHABIKI WETU AMBAO KIMSINGI NILIWAELEWA AND I TOOK EVERYTHING AS A MAN...
“BADO NASIMAMIA KUWA CHOCHOTE NILICHOFANYA NILIAMINI KUWA NILIKUWA NAFANYA KITU POSITIVE,LAKINI KUMBE WENZETU HAWAKUWA NA NIA NJEMA WALA DHAMIRA YA KWELI YA KUTAKA MUAFAKA BALI WALIKUWA NA AJENDA ZAO ZINGINE,MAANA MPAKA LEO HII HAKUNA HATA MOJA WALILOTEKELEZA KUTOKANA NA ULE MUAFAKA.“NA ZAIDI MARA WANAKUJA NA HILI LINGINE LA KUWASHTAKI MAPACHA NA HUKU NI WAO WALIOSEMA TUNAANZA 'MWANZO MPYA'...AMBAPO MIMI NILISEMA HAKUNA VITA ISIYOKUWA NA MALENGO NA NILIAMINI KWA DHATI MALENGO YETU SASA YALIKUWA YAMETIMIA...SASA WAO WANAPOJARIBU TENA KUVURUGA UTEKELEZAJI WA MALENGO BASI HAKIKA MALENGO YANAKUWA HAYAJATIMIA NA MAPAMBANO 'INALAZIMIKA' YAENDELEE...”