Google PlusRSS FeedEmail

VURUGU ZASABABISHA KUSITISHWA KWA SHOW YA DIAMOND

Tukio la vita na mauaji lilitokea wiki kadhaa zilizopita mjini  Songea mkoani Ruvuma, limemtibulia ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul na kushindwa kufanya shoo pande hizo
Akizungumza na ripota wetu baada ya kurejea jijini Dar es Salaam, akitokea mkoani humo, Diamond alisema alichukuliwa na promota aliyemtaja kwa jina moja la Eddo kwa ajili ya kwenda kufanya shoo katika Ukumbi wa Jambo Lee, Songea mjini, lakini ilishindikana kutokana na taarifa ya polisi kuwa hakuhitajiki mkusanyiko pande hizo.“Nilifikia hotelini na kikosi changu cha kazi, niliambiwa maandalizi yamekamilika na tayari watu 800 walishakata tiketi, muda wa shoo ulipofika nilishangaa sipigiwi simu, ndipo nilimtafuta mhusika akaniambia imeshindikana kwa sababu za kiusalama, nikapewa Sh. milioni moja nikarudi Dar na bado nadai Sh. milioni mbili.“Kilichosababisha yote hayo ni mauaji yaliyotokea siku za nyuma na vita kati ya polisi na raia, lakini mashabiki wangu wasijali waendelee kunipigia kura ili nishinde Tuzo za Kili kwa kutuma neno Kili B1, Kili C2, Kili F3, Kili R1, Kili U1, Kili V3, Kili V4 kwenda namba 15747,” alisema Diamond.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging