Google PlusRSS FeedEmail

BIFU JINGINE NDANI YA KUNDI LA MEXICANNA LA CAVERA

Msanii wa zamani wa Kundi la Mexicanna La Cavera, Baghdad, leo amesema yeye yuko tayari kufikishwa mahakamani ama mbele ya mkondo wa sheria na wasanii wenzake waliobakia kwa kuwa yeye anayohaki ya kumiliki na kutumia nembo ya Mexicana kibiashara.Akiongea kwenye kituo cha Kituo kimoja cha  Radio Mwishoni mwa wiki ,Baghdad alikuwa akijibu tuhuma ambazo ziko mtaani kuhusu mtafaruku na mtifuano kati ya wasanii hao ambapo msanii alisema yeye ndiye alilipia “Plates” ama sahani zinazotumika kuchapa nembo mbali mbali.“ Mimi ndiye niliyelipia plates hizo na baada ya msanii Baghdad kujitoa sisi hatukumchukulia hatua za haraka haraka kumdai vitu vya Mexicanna La Cavera kwa sababu alikuwa anaumwa sana. Baadae tulipomfuatilia Baghdad tukaona ameanza kutumia nembo yetu kwenye mtandao wa Facebook akinadi fulana zake’, alisema mmoja wa wasanii wa kundi hilo.Baghdad alimaliza kwa kusema,’Siongei na mshika kamba mbwa bali naongea na mwenye mbwa mwenyewe’.Sasa bado haijajulikana kwa jinsi utata huu ulivyo ni nani mwenye mbwa ama mmiliki halali wa kundi hilo...

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging