Tangu jana kitaani na kwenye mitandao ya kijamii kumekuwepo na rumors juu ya kifo cha muigizaji na Director wa filamu Sajuk , Kutokana na taarifa hiyo lawama zote zikamuangukia Actor ambaye pia
ni mwimbaji wa Bongo Flava Hemedy ambaye inadaiwa ndiye aliyeandika taarifa hizo kwa mara ya kwanza katika status yake ya facebook kuwa Sajuk ameaga dunia.. Hemedy amesema yeye hausiki kabisa nakuandika taarifa hizo ila kuna mtu amefungua ukurasa katika mtandao wa facebook kwa jina la Hemedy na kuandika ujinga huo ila nini kauli ya Sajuk "napenda kuwaambia mashabiki wangu ni kweli naumwa ila kwa sasa hali si mbaya sana naendelea vyema na kwa sasa niko location nafanya filamu yangu mpya .niliposikia habari kwamba nimekufa kweli zimenishtua sana ila napenda kuwaambia maadui zangu kwamba kama mwenyezi Mungu akipenda na wakati utakapofika atachukua uhai wangu ila sitakufa kwa maneno yao,"Wapenzi wangu kaeni mkao wa kula maana filamu yangu mpya iko njiani alimazia Sajuki "Nae mke wa sajuki alikuwa na haya ya kusema "Ninaomba wadau wa filamu pamoja na Watanzania wote kutuchangia fedha kwa ajili ya matibabu ya Sajuki mume wangu ambaye ni mhimili mkubwa katika familia yetu na jamii nzima kwa ujumla fedha inayohitajika ni nyingi sana, mchango wako ni muhimu sana tunatanguliza shukrani zetu kwenu nyote mnayeguswa na tatizo hili,Kwa wale wanaoguswa na msanii huyu tunaomba wachangie michango hiyo kwa kupitia Tigo – Pesa kwa namba 0713 666 113 Wastara Juma pia unaweza kutama fedha hiyo kwa kutumia Akaunti namba 050000003047 Akiba Commercial Bank.