Google PlusRSS FeedEmail

"KAJALA"MH HAKIMU SEGEREA KUNATISHA SANA


Aliweza kutoa shinikizo hilo mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo, muda mfupi baada ya wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU), Leonard Swai, kuikumbukusha mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja jana kwa ajili ya upande wa jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao, lakini akadai hilo halitaweza kufanyika, kwa sababu hajaja na mashahidi na anaomba kesi hiyo iahirishwe.

Kwani kesi hiyo humkabili msanii wa Filamu hapa nchini, Kajala Masanja na siku chache zilizopita aliweza kumwaga machozi huku akiujia juu upande wa Jamhuri kwenye kesi inayomkabili ya usafishaji fedha haramu ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hapa Jijini.Baada ya wakili huyo kumaliza kutoa maelezo hayo, ndipo Kajala akanyosha kidole na kuomba ruhusa ya mahakama ili aweze kuzungumza jambo.
Msanii huyo alipata mwanya wa kuongea na Mheshimiwa Hakimu huku akibubujikwana machozi na kusema kwamba, "Hivi huyu wakili wa serikali anafikiri kule Segerea ninakoishi kwa sasa ni sehemu ya starehe? Mahabusu kunatisha, wewe wakili wa serikali lete mashahidi kesi isikilizwe,”Mbali na hilo Hakimu Fimbo aliwezakuhairisha kesi hiyo hadi kufikia Mei 9, ambapo upande wa jamhuri unatakiwa ulete mashahidi wake ili waanze kutoa ushahidi.
Ilidaiwa na Wakili Swai kwamba Machi 27 mwaka huu mbali na mshitakiwa Kajala...mshitakiwa mwingine ni mumewe Faraja Chambo, wanakabiliwa namakosa matatu.Alisema kosa la kwanza linalowakabili washitakiwa hao ni pamoja na kula njama kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa ya mwaka 2007, ambapo wote wawili walitenda kosa hilo la kula njama la kuhamisha umiliki wa nyumba iliyoko Kunduchi Salasala eneo ambalo halijapimwa hapa Jijini.Kosa la pili ni kwamba Aprili 14 mwaka 2010, walihamisha isivyo halali umiliki wa nyumba hiyo, ambayo walikuwa wakiimiliki kwenda kwa Emilian Rugalia, ambaye ndiye waliyemuuzia kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya TAKUKURU ya mwaka 2007. Na shtaka la tatu ni la kutakatisha fedha, ambalo walilitenda siku hiyo ya Aprili 14, 2010 huku wakijiua ni kinyume cha sheria hiyo.Mshitakiwa Chambo naye yuko mahabusu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, kwa sababu anakabiliwa na kesi nyingine ya utakatishaji fedha haramu, iliyofunguliwa mahakamani hapo, ambapo kwa mujibu wa sheria, kosa hilo halina dhamana.

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging