Google PlusRSS FeedEmail

KILL KUFUNGA MTWARA LEO

Tamasha la kufunga maonyesho ya washindi wa tuzo Kill Music, linatarajiwa kuhitimishwa leo kwenye viwan ja vya Umoja mkoani Mtwara. Onesho hilo linatarajiwa kuwa la aina yake kutokana na kushirikisha wasanii ambao ni washindi wa tuzo za Kill Music waliozuru katika mikoa mbalimbali nchini .Akizungumza Dar es Salaam jana Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, alisema kuwa kilele chake kinatarajiwa kuwa jijini Dar es Salaam wiki ijayo .Alisema tamasha hilo litafunga dimba kwa mikoani ambapo wakazi wa Dar es Salaam wakae mkao wa kula kwa ajili ya tamasha la mwisho. Alisema lengo kubwa la tamasha hilo ni pamoja na kuibua vipaji na kuwafanya wasanii chipukizi kufikia malengo kwa kurekodi nyimbo zao katika studio za kisasa.Alisema pia washindi wa tuzo za Kill, wanapata fursa ya kutoa shukrani kwa washabiki wao wa mikoani kutokana na kujua mchango wao na kuweza kuwapigia kura....

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging