Google PlusRSS FeedEmail

MSHINDO NA PENINA NI BALAA KATIKA HARAKATI.

Mshindo Jumanne, muigizaji na mtayarishaji wa filamu mwenye fani lukuki amekamilisha filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la HARAKATI, Mshindo ambaye miezi kadhaa iliyopita alinukuliwa kuwa hatoandaa filamu zake mwenyewe na badala yake atafanya kazi za kampuni fulani jana ameyakana maelezo yake hayo na kusema kuwa sasa atasimama na kampuni yake ya SSG DISTRIBUTORS tu.Na hana mpango wa kushirikiana au kufanya kazi za kampuni nyingine zaid ya SSG,kwani alipokuwa katika kampuni nyingine ilikuwa katika suala la utatfiti wa mambo mbalimbali ya tasnia ya filamu kwa sasa anaamini kuwa amepata shule ya kutosha.“unajua kaka nina ndoto na fikra nyingi katika akili yangu sasa sometime inakuwa inaumiza pale mawazo yako yanapokuwa yanapuuzwa sababu ya vitu fulani fulani ambavyo kimsingi havina maana hivyo nimeona ni bora niendeleze jeshi langu na naamini nitapata mafanikio zaidi. Baada ya Mshindo kuacha kuandaa kazi zake mwenyewe na baadae kurudi kufanya hivyo,mara ya kwanza alifanya hivyo kwa kuzipa umiliki filamu zake kampuni ya Steps na baadae mwishoni mwa mwaka jana alidondokea Sharks video production.
                                                           
                        
                                                Penina akiwa Mshindo katik pozi.
Kwa sasa Mshindo amesema ataendelea kushirikiana kwa mawazo na ushauri ila hatoandaa kazi chini ya lebo ya kampuni yoyote labda kama kampuni hiyo inunue kazi yake yake ikiwa imeshakamilika tena kwa kwa maslahi yanayomlipa Mshindo ni mmoja wa wasanii waliopata mafanikio makubwa kwa kusambaza wenyewe kazi zao kwa miaka saba katika tasnia ya filamu amefanikiwakutayarisha na kusambaza filamu zaidi ya 24. Sasa anakuja na filamu ya Harakati ambayo yeye anasema ni moto wa kuotea mbali filamu hiyo iliyobeba kisa mahsusi kinachogusa mambo ambayo yanatendeka katika jamii kila siku ijapokuwa ,amesisitiza kisa hicho ni cha kubuni tu hakihusiani na mtu yoyote.Mshindo anasema kisa hicho kama kitamgusa mtu yoyote basi amuwie radhi,wasanii wengine walioshiriki katika filamu hiyo ni Rashid Wazir (bubu wa filamu ya zuadiswa) ambapo katika filamu hiyo ameuvaa vizuri uhusika wa msukule, Jenifer Raymond (Penina) Sadikina Mussa ambaye ni wazi kabisani tishio kwa wasanii wengine Fikiri Salum (Beno) Halima Mponera na Mshindo wenyewe.Mshindo amesema kuwa alikuwa akitamani sana kufanya kazi na msanii kama Wema Sepetu kitambo lakini kwa sasa amempata Sadikina ambaye anafanana na wema lakini inawezekana akawa mkali kuliko Wema.

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging