Google PlusRSS FeedEmail

SKENDO ZAZIDI KUWEKA PENZI LA DIAMOND PABAYA WAKWE WAMJIA JUU

Skendo ya kunaswa hotelini na mcheza sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel bado inamtesa mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’ ambapo safari hii anadaiwa kuchafuka vibaya upande wa wakwe zake kwa mchumba’ke Jokate MwegeloHabari kutoka kwenye chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao zinadai kuwa baada ya habari hiyo kubumburuka, imekuwa ngumu kumsafisha Diamond ukweni.
MSURURU WA WANAWAKE
Ilidaiwa kuwa habari hiyo ndiyo iliyotonesha kidonda kilichokuwa kinataka kukauka cha ‘kichaa’ huyo wa Bongo Fleva kutajwa kutoka kimapenzi na msururu wa wanawake mastaa na wasiokuwa mastaa.“Asikwambie mtu, unajua upande wa akina Jokate ni watu wa dini sana. Yaani kwa skendo skendo kama hizo, wanamuona Diamond kama anataka kuwachafua.“Unajua zile ishu za kudaiwa kutoka kimapenzi na msururu wa wanawake zilikuwa zimeanza kutulia kwa sababu yupo na Jokate lakini baada ya kutokea hii ya kunaswa hotelini na Aunt, imetibua mambo kule ukweni na mbaya zaidi anaonekana hajatulia,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutochorwa jina.
HUYU HAPA DIAMOND
Diamond alipogonga stori na ripota wetu alisema kuwa anahisi kuna watu nyuma ya habari hizo ambao wamelenga kumharibia mambo yake.“Naomba niweke wazi jambo hili kwa sababu ni kweli nachafuliwa.“Kuna watu wananichafua ili nionekane kituko kwenye familia ya akina Jokate, nahisi wanaweza kufanikiwa,” alisema Diamond Platnumz.
UHUSIANO WAKE NA JOKATE
Kufuatia ishu hizo, uhusiano wa kimapenzi wa kidume huyo na mwanamitindo Jokate unadaiwa kuwa kwenye hatihati pamoja na kwamba bado wapo pamoja.
TULIKOTOKA
Mwishoni mwa wiki iliyopita Diamond na Aunt walidaiwa kubambwa katika Hoteli ya Kebby’s iliyopo Mwenge, Dar wakila ‘good time’, hivyo kuzua tafrani kwenye uchumba wa mwanamuzi huyo na Jokate.Mbali na madai hayo yanayomhusisha Diamond na Aunt ‘kuminya’ pamoja, kichwa hicho cha Bongo Fleva kiliwahi pia kutajwa kutoka na mwigizaji Jacqueline Wolper, wauza nyago kwenye video za muziki, Rehema Fabian na Natasha, staa wa Maisha Plus, Pendo Moshi kabla ya kumchumbia Wema Sepetu kisha wakamwagana na kujikuta mikononi mwa Jokate.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging