MWIGIZAJI Chipukizi katika tasnia ya filamu Sadikina Mussa anasema kuwa katika tasnia ya filamu hana mpinzani kabisa angalau kidogo mtu ambaye anaweza kwenda naye sambamba na kumfikia katika uigizaji kwa wasanii wa kike ni Wema Sepetu tu ndio anayemuona anaweza kushindana naye katika fani hiyo ya uigizaji. “Sioni kama kuna msanii wa kike mwenye uwezo wa kuigiza kama mimi katika tasnia ya filamu kwa sasa, kwani wasanii wengi mara nyingi wapo vile vile hawabadiliki, mpinzani tena kidogo labda anaweza kuwa Wema Sepetu, Wema uigizaji wake ni wa uhalisia kama sura ninayo pia mvuto ninao na najua kuigiza,”anasema Sadikina.Msanii huyo ambaye ameshiriki katika filamu kadhaa hivi sasa anakuja na filamu ya Harakati kutoka kampuni ya SSG Distributors, msanii huyo ambaye amefanana kimuonekano kama Wema Sepetu ni kipaji kilichovumbuliwa na Mshindo Jumanne, katika filamu ya Harakati ameigiza kama mhusika mkuu...
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.