Google PlusRSS FeedEmail

WOLPER KUIMBA TAARABU

Msanii mwenye mvuto ndani ya bongo movie Jackline Wolper, huenda akazamia kwenye uimbaji wa taarabu, kwani ukaribu aliokuwa alionao na wasanii wa tasnia hiyo unazua hofu kubwa . Kwa sasa kuna wimbi kubwa la wasanii wa tasnia ya bongo movie waliozamia kwenye tasnia ya muziki , huku wakisubili miujiza ya kuweza kuwateka akili mashabiki..Naye msanii huyo inaonekana kuupenda sana muziki huo wa taarabu ingawa mwili wake pamoja na mikogo yake haifanani kabisa na aina ya muziki. 
Msanii huyo alikaririwa na mwandishi mmoja wa hapa jijini kuwa si kwamba anakipaji cha uigizaji pekee bali hata uimbaji, mitindo na mambo mengine kama kufanya biashara .Alidai kuwa watu watashangaa endapo ataamua kuchukua maamuzi hayo ya kuzama kwenye taarabu lakini hataimba kwa kutaka fedha tu kwani uwezo alikuwa nao kifedha unamtosha ingawa bado anaendelea kuzisaka “Naendelea kuzisaka chapa kwani nimekuja mjini si kushanga magorofa au kujenga bifu na watu, nimetumwa kutafuta fedha katika kazi zangu na si kwa biashara chafu” alidai

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging