Google PlusRSS FeedEmail

WEMA AMSAIDIA DIAMOND KUZUNGUMZA KIINGEREZA

Msanii wa muziki Naseeb Abdul ‘Diamond Plutnam’ amekiri hadharani aliyekuwa mpenzi wake Wema Sepetu kuwa amempa uwezo mkubwa wa kuongea kiingereza. Diamond aliyatamka hayo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha televisheni ambapo mtangazaji alimpongeza kwa kuongea kingereza bila ya kutetereka katika shoo yake aliyoifanya katika jumba la Big Brother hivi karibuni nchini Afrika Kusini...
Baada ya kupongezwa Diamond alisema uwezo huo alipewa na Wema wakati wa mapenzi yao ambapo msanii huyo wa filamu mara nyingi hupenda kuzungumza Kingereza tofauti na Kiswahili hivyo yeye kutumia nafasi hiyo kama kujifunza kwake . “ Nasema Wema ndio amenipa uwezo mkubwa wa kuongea kiingereza bila ya kutetereka nadhani ningepewa nafasi ya kumshukuru kwa hili ningemshukuru sana kwani amenipa funzo kubwa “ alisema
Diamond hivi karibuni aliangusha shoo ya nguvu katika jumba hilo ambapo baada ya hapo alifanya mahojiano na hapo ndipo aliwakosha watanzania wengi nah ii ni mara ya pili kwa wasanii watanzania kupata fursa ya kwenda kuhudhuria katika jumba hilo

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging