Google PlusRSS FeedEmail

EDDIE MURPHY ANOGEWA NA PENZI LA MTOTO

MCHEZA filamu mkali Eddie Murphy ambaye kwa sasa ana miaka 51, aliamua kujitakatisha kitaani akiwa na mpenzi wake Rocsi Diaz, 28. Miaka 51 na 28 ni tofauti kubwa kwa wawili hao kwani wanaweza kuwa baba na mwana, lakini wao hawakujali kwa malavidavi ya kufa mtu waliyokuwa wakipeana mtaani.
Murphy anayejulikana zaidi kwa kucheza filamu za vichekesho, alikuwa katoka kupata 'gahawa' na mpenzi wake huyo aliye mtangazaji wa kituo cha BET.Wakati wanatoka walianza kukumbatiana na kubusiana, bila kujali macho ya watu kibao yaliyokuwa yakiwatazama.Murphy alionekana ni mwenye furaha zaidi kwa muda wote, huku akijaribu pia wakati mwingine kujiziba sura ili watu wasimjue.Ndivyo hivyo tena, penzi linaonekana lishamkolea.Msanii huyo ana watoto watano, aliowapata kutoka kwa mke wake wa zamani, Nicole Mitchel na ana mtoto aliyezaa na aliyekuwa mwanamuziki wa kundi la Spice Girl, Melanie Brown

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging