Sanaa ya muziki wa kitanzania ina asilimia 17 katika soko la muziki wa kimataifa kutokana na wasanii kutojiandaa kupeleka kazi zao katika soko hiloKauli hiyo ilitolewa na Meneja wa Bendi ya Njenje, John Kitime wakati alipokuwa anaongea na waandishi wa habari na wadau wa sanaaKitime alisema baadhi ya wasanii wanatoa albamu moja na kutangaza kutaka kufanya muziki kimataifa wakati hawajianda katika ngazi hiyo
Alisema kuwa wamekosekana watu wenye mtazamo wa kufanya soko la sanaa kuwa la kimataifa na kuifikisha sanaa mbali pamoja na kumnufaisha msanii kwa kupata kipato kinachoendana na kazi yake Kitime alieleza kuwa kuna baadhi ya wasanii wanaoenda njee kwa ajili ya kufanya shoo lakini wanaishia kupigia kwenye hadhira ya watanzania pekee yao kwa sababu matayarisho yao ni kwa WatanzaniaB Pamoja na hayo alitoa wito kwa wasani kuwa na menejimenti, kuangalia wenzio wamefika wapi kuiga mazuri yanayofanywa na wasanii wengine, pamoja na kuwa na nidhamu ya muda Aliongezea kuwa kutokana na utandawazi wasanii wawe na tabia ya kujiuza wenyewe kwa kutumia mitandao..