Inawezekana ukawa una taarifa kwamba Diamond ni msanii mwenye Fedha nyingi hapa Tanzania kutokana na show za bei gali na nyingi anazozifanya. Inawezekana ukawa unataarifa kwamba Diamond ndio msanii ambae yuko juu kwa sasa Tanzania, na kwamba ndio msanii aliepiga show nyingi za bei ghali mwaka jana. siyo hayo tu… kuna uwezekano ukawa una taarifa zake nyingi tu lakini hili ninalotaka kukwambia mimi ndio kwanza unalisoma kutoka hapa. Akiongea na kituo kimoja cha radio hapa nchini amekubali kuzungumzia nyumba yake anayoijenga Tegeta Dar es salaam kutokana na pesa za muziki. Amesema “ninapopata huwa najaribu kutengeneza vibanda vyangu vinisitiri manake ninazo nyumba tofauti tofauti, nyumba ya Tegeta nimetumia milioni 69 mpaka sasa, ni ya vyumba vinne titatu ni Master, kuna jiko kubwa tu, choo cha public, studio, dining, sitting room… ni nyumba ya kisasa, kiwanja nilikinunua mwezi wa tisa 2011, nyumba nyingine ninazojenga zipo zipo ila huwa sipendi kuzizungumzia”..
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.