SELENA GOMEZ AFANYA MAHOJIANO NA POLISI
Rafiki wa kike wa mwanamuziki kinda Justin Bieber, Selena Gomez atahojiwa na polisi kuhusu (Bieber) kumshambulia mpiga picha maarufu kama paparazi,kwa mujibu wa taarifa. Bieber anatakiwa kuhojiwa na polisi wa upepelezi wa Los Angeles, baada ya mpiga picha kulalamika kuwa mwanamuziki huyo wa pop alimshambulia akiwa dukani.” Tunataka kufanya mahojiano na kila mtu na yeyote anayehusika na upelelezi huu, “ msemaji wa polisi, Steve Whitmore aliliambia gazeti la New York Daily News.
Askari mwenye cheo cha Luteni,Robert Wiard alisema mpiga picha alipiga simu kwa polisi akitumia namba 911, jumapili akilalamika kupigwa na kupata maumivu katika kifua chake.
Wiard alisema balaa lilianza wakati mpigapicha huyo alipotaka ‘kumfotoa’Bieber aliyekuwa na Gomez, baada ya kutoka nje ya jumba la sanaa la The Commons lililopo eneo la Calabasas.
Alisema mpigapicha huyo alipelekwa hospitali ambako alitibiwa na kuruhusiwa. Wiard alisema, Bieber alikuwa na Gomez baada ya kutoa kipondo hicho walitimka kwa hiyo polisi wanataka kufanya uchunguzi kwa kumhoji ili kupata maelezo ya pande wa pili
Wakati huohuo, wimbo mpya wa Bieber ‘Die in Your Arms’ uliopo katika albamu yake mpya ya ‘Believe ‘unatoka Jumatatu