Google PlusRSS FeedEmail

MH. MAKALA ATOA RAMBIRAMBI KWA KANUMBA

                              
SERIKALI imetekeleza ahadi iliyotoa wakati wa msiba wa gwiji la tasnia ya filamu  Marehemu Steven Kanumba, zoezi hilo lilifanyika nyumbani kwa marehemu Kanumba Sinza Vatcan City, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Amos Makalla aliwakilisha serikali kutoa rambirambi ya shilingi milioni 10, kwa familia ya Marehemu Kanumba.Pamoja na kutoa rambirambi, Naibu Waziri Makalla alisisitiza kuwa kifo cha Kanumba kimeleta chachu na kuahidi kuwa serikali itajikita kikamilifu kusimamia kuboresha pato la wasanii wote ikiwa wasanii wa filamu ambao mara nyingi jamii imekuwa ikiwaona kama ni watu wenye maisha ya kitajiri kumbe ni tofauti na ukweli halisi. Mama yake na marehemu Kanumba akiwa na fedha alizopokea kutoka kwa Serikalini pichani kulia ni Naibu waziri Mh. A.Makala.
“Serikali imejifunza kupitia kifo cha Msanii wetu aliyelitangaza Taifa kwa kazi zake lakini hajafaidi kabisa jasho lake kutokana na wizi wa kazi zao, serikali inapanga mipango itakayotoa fursa kwa wasanii kufaidika na kazi zao,”alisema Mh. Makala.Naye mama wa Marehemu ameishukru Serikali kwa kumuunga mkono katika kipindi kigumu cha msiba mwanaye kwani amepata changamoto nyingi kutoka kwa mzazi mwenzake huku hata jamii ikijaribu kuamini kuwa marehemu Kanumba alikuwa na mali nyingi kulingana na kazi alizofanya kumbe hakuwa na fedha hizo zinzohisiwa.“Kweli inakatisha tamaa sana mwanagu kaigiza filamu 42 lakini kama kuanza kujitegemea ameanza mwaka 2010 tu, maisha yake yote alikuwa akiishai kwangu kupanga hata miaka miwili hajamaliza ina maana angefika mwezi wa saba ndio ingekuwa miaka miwili Naishukru sana Serikali kwa kunisaidia kwa kila hatua,” anasema mama Kanumba.

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging