Wapenzi Kanye West na Kim Kardashian, hivi sasa wamebainisha kwamba wapo kwenye hatua ya maandalizi ya kufunga ndoa ili waanze kuwa na watoto. Kwa mujibu wa marafiki wa wapenzi hao, Kanye kwa sasa anafikiri kuwa na watoto na mpenzi wake huyo
Gazet la US Weekly limeandika kwamba Kanye na Kim hivi sasa kwa pamoja wameamua kuanzisha familia na kuna uwezekano wakafunga ndoa hivi karibuni . "Kanye anafikiria zaidi kuwa na watoto na mpenzi wake Kim na hivi sasa wapo kwenye maandalizi makubwa ya ndoa yai" kilisema chanzo kimoja kilichonukuliwa na gazeti hilo
Katika kuhakikisha kwamba hawafanyi utani, wapenzi hao hivi sasa wamehamia katika jumba moja la kifahari hapa Los Angles, ambalo wanaishi pamoja