KIM AIBIWA VITU VYENYE THAMANI KUBWA
Mtangazaji Kim Kardashian amesema mfanyakazi mmoja wa shirika la ndege la Britsh Airways, amemuibia vitu vyake ambavyo haviwezi kurejeshwa kwa pesa, wakati aliporejea nyumbani kwake akitokea Ufaransa,ijumaa usiku aligundua kuwa mfuko wake ni mwepesi tofauti na alivyokuwa mwanzo.
Baada ya kufanya uchunguzi katika mkoba wake aligundua kuwa wezi walimuibia miwani aliyoachiwa na baba yake, Robert Kardashian, ambayo alimpa kama zawadi kabla hajafariki na vitu vingine. Kim aliamua kuandika katika ukurasa wake wa tweeter kuwa”Nimeudhika sana na shirika la British Airways, walivyofungua mfuko wangu na kuchukua vitu vyangu muhimu na vingine siwezi kuvipata tena”
Tayari Kim ameshapeleka malalamiko yake katika shirika hilo kutokana na tukio hilo na amedai kuwa kama huko hatopatiwa ufumbuzi atakwenda polisi.