Google PlusRSS FeedEmail

VINARA TUZO KILL KUONYESHANA KAZI LEO

Washindi wa tuzo za Kill Music wanatarajia kufanya oneshi la aina yake leo katika viwanja vya posta, Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema onesho hilo linatarajiwa kuwa la aina yake kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya. Alizema onesho ilitashirikisha wasanii wote walioshinda katika tuzo za Kill zilizofanyika mwaka huu ambazo zinadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia Bia yake ya Kilimanjaro.Kavishe alisema baada ya kufanyika tuzo za mwaka huu waliunda timu ya wasanii ambao walizunguka mikoa sita ya Tanzania bara kwa ajili ya kutoa shukurani kwa wadau na wapenzi wa muziki nchini kwa kuwapigia kura.Alisema katika ziara ya mikoani pia waliwashindanisha wasanii chipukizi ambapo washindi watakuwepo katika onesho la leo pamoja na kupewa ofa ya kurekodi nyimbo katika studio za kisasa.Meneja huyo aliwataja wasanii watakaotoa burudani katikaonesho la leo ni pamoja na Diamond,Dimpoz, Queen Darlin,Suma Lee, Twanga pepeta, Khadija Kopa, Ally Kiba, Ben Pol, Barnaba, AT, pamoja na Roma Mkatoliki ambapo kiingilio kitakuwa sh. 4000

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging