Google PlusRSS FeedEmail

MARIO VAN PEEBLES KITOKA HOLLYWOOD KUTINGA NDANI YA TAMASHA LA ZIFF

Gwiji wa utengenezaji wa filamu Hollywood Mario Van Peebles anatarajia kuwa ni mmoja kati ya watengenezaji wakubwa wa filamu ambao wanatarajia kushiriki katika tamasha kubwa la filamu la Zanzibar International Film Festival (ZIFF) mtengeneza filamu huyo ujio wake ni faraja na faida kwa wasanii wa hapa Nchini, tamasha la 15 kufanyika.Mario Van Peebles ameshiriki filamu kama Ali mwaka 2001, filamu ya New Jack City 1991, Posse mwaka 1993, Baaadasss 2003 pia mtayarishaji huyo ameongoza filamu zaidi ya 27 na kushiriki katika kuigia filamu kama 87 Hollywood pia akiwa amechaguliwa na kushiriki katika tuzo mbalimbali na kushinda....Mario Van Peebles...Kitaaluma ni mchumi elimu yake ya uchumi aliipata katika chuo Kikuu cha Columbia huko Marekani, katika tamasha la ZIFF kwa upande wa burudani wasanii wanaotarajia kutumbuiza ni Dj Cleo kutoka Afrika ya Kusini, Cabo Snoop kutoka nchini Angola, The Mushrooms (Kenya), kutoka Tanzania ni Diamond, Roma, Lady Jay Dee, Barnaba, Ali Kiba na Mashauzi Classic.
                               Zanzibar International Film Festival.
Tamasha la ZIFF litaanza rasmi tarehe 7 hadi 15 mwezi Julai 2012 tamasha linalotarajia kukusanya watengenezaji wa filamu utoka kila kona na kuandika historia ya tasnia ya filamu Afrika Mashariki na kati na mataifa mengine makubwa yatengenezayo filamu yatashiriki.

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging