Google PlusRSS FeedEmail

MASHUJAA KUTAMBULISHA NYIMBO MPYA KANDA YA ZIWA




Bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa ‘Wana kibega’inatarajia kufanya ziara maalumu kwa mashabiki wake wa kanda ya Ziwa mwishoni mwa wiki . Akizungumza Dar es Salaam jana Meneja wa bendi hiyo Martin Sospeter alisema onesho la kwanza litafanyika Ijumaa mjini Kahama mkoani Shinyanga

Alisema jumamosi watatoa burudani mjini Geita na Jumapili watakuwa jijini Mwanza. Meneja huyo alisema wameandaa shoo ya nguvu kwa wapenzi wa mikoa hiyo ikiongozwa na Lilian Internert, akiwa na wengine ambao wataonesha shoo zao mpya zilizoundwa hivi karibuni

Sospeter alisema katika maonesho hayo nyimbo zao zote zitapigwa ikiwa ni pamoja na zilizokuwa hazijawahi kusikika kwenye vyombo vya habari “Kuna ngoma mpya ambazo zitaanza kusikika huko huko tutafanya kama kuwatambulisha wapenzi wa kanada ya ziwa waone mambo mapya ya Mashujaa” alisema

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging