MSONDO KUZINDUA EMIRATES
Bendi kongwe ya muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma ya jijini Dar es Salaam inatarajiwa kufanya uzinduzi wa ukumbi mpya wa burudani Emirates uliopo Masasi Mtwara huni 2, mwaka huu kwa lengo la kufanya shoo zao.
Akizungumza Dar es Salaam jana msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila alisema wamealikwa kutoa burudani siku ya ufunguzi wa ukumbi huo, ambapo wamepania kutoa burudani ya nguvu "Unajua sisi ni Baba ya Muziki nchini, ndio maana wapenzi wengi wa dansi wanahitaji burudani kutoka kwetu" alisema