Google PlusRSS FeedEmail

PENZI LA KIM NA KANYE WEST LAZIDI KUCHANUA

Kim Kardashian na Kanye West wamekwenda katika hatua nyingine ya mahusiano yao, baada ya kuanza kujianda kuishi pamoja.Wapendanao hao walianza kuzimikiana miezi mitatu iliyopita na wote kwa sasa wameamua kuuza makazi yao yaliyopo jijini Los Angeles, ili waweze kutafuta mahali watakapofaidi penzi lao.
Vyanzo vya habari vililiambia jarida Life & Style "wanajiandaa kuishi pamoja na walipanga jambo hilo kwa haraka na endapo jambo hili likiendelea kwa kasi kama hii Kim na Kanye wanaweza kupanga nyumba mpya kwa pamoja". Vyanzo hivyo vya habari vinaeleza kwamba Kim ambaye alitengana na mumewe Kris Humphries Oktoba mwaka jana zikiwa ni takribani siku 72 za ndoa anaiuza nyumba yake iliyopo maeneo ya Beverly Hills Villa kwa dola milioni 5 ,Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ.com Kanye alishaliweka sokoni jumba lake lenye vyumba vitatu lilopo katika eneo la Hollywood Hills, ambalo alilinunua mwaka 2003 kwa dola 3,995,000 lakini hadi sasa hajawahi kuliuza

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging