Google PlusRSS FeedEmail

PROF. JAY WANAMUZIKI WAKONGWE WAMESAHAULIKA

Watanzania wamesahau muziki wa kizazi kipya umetoka wapi wanashindwa kuheshimu watu waliotoa muziki na kuufanya ukubalike katika jamii yetu. Kauli hiyo ilitolewa na mwanamuziki mkongwe wa kizazi kipya Profesa Jay alipokuwa anafanya mahojianao kwenye kituo kimoja cha televisheni jijini
Alisema kuwa wanashindwa kuheshimu walioutoa muziki mbali kama Sugu ni msanii ambaye ameutoa muziki mbali na ni msanii wa kwanza kutoa albamu 12 hivyo anatakiwa kupewa heshima kwani amehangaika na kuupigania muziki"Wanapewa heshima wa sasa na kuwasahau wakongwe,unashindwa kumheshimu babu na unamheshimu mjukuu hii haileti maana kwani hata mjukuu huyo hataweza kumheshimu babu yake,"alisema  Profesa Jay Mbali na hayo Profesa alisema watu wengi wanamshauli kuingia katika siasa kwani anaishi mtaani kama kiongozi, na wasanii wa Bongo Fleva wanamchukulia kama kiongozi wao. Alisema kuwa anachukia siasa kwa sababu ina mambo mengi ya uongo, na hapendi kudanganya hivyo akiingia kwenye siasa atalazimika kudanganya, na akibaki kwenye ukweli itamletea matatizo Kwa upande wa mahusiano alisema kuwa alikuwa na mahusiano na Rashida Wanjara lakini wameachana kwa amani na anauwezo wa kumsaidia jambo lolote lile ambalo liko ndani ya uwezo wake. Alisema bado hana ndoto za kuoa kwa sasa ingawa anamtoto wa miaka 9

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging