SHARON APAGAWA NA PENZI ANALOPEWA NA MARTIN
Kweli kupenda ni upofu! Mcheza filamu aliye na jina Sharon Stone, ameonekana kupagawa mno kwa penzi analopewa na dogo.Sharon alidhihirisha hilo, wakati wawili hao walipoonekana wanakata mitaa ya Beverly Hills jana wakiwa katika mtindo wa 'zero distance'.
Mkongwe huyo alionekana kila mara anambusu na kumkumbatia dogo wake, aliyemzidi mno umri, Martin Mica wakati wakikatisha mitaa. Sharon, 54, alianza mahusiano na mvulana huyo raia wa Argentina ambaye ni mwanamitindo, wakati walipokutana Brazil Aprili mwaka huu.
Inadaiwa baada ya kukutana, saa chache baadaye wawili hao wakatumia muda mwingi wamejifungia ndani ya chumba cha hoteli aliyokuwa amefikia Sharon.Martin, umri wake ni nusu ya Sharon, alionekana hana hofu yoyote, huku naye akimwaga malavidavi ya kufa mtu kwa demu wake.Hii si mara ya kwanza kwa wawili hawa kuonekana wakifanya mambo hadharani.