WAKALI wa tuzo za muziki za Kilimanjaro mwaka 2012, juzi walidhihirisha uwezo wao mbele ya mashabiki lukuki, waliyohudhuria kwenye Viwanja vya Chuo cha Posta kuwashuhudia wasanii hao waliyowapigia kura na kunyakua tuzo hizo.
Mashabiki hao waliofurika kwenye viwanja hivyo vya Posta, walishuhudia wasanii 12 na bendi mbili waliyotwaa tuzo wakilishambulia jukwaa.
Onesho hilo lilikuwa ni hitimisho la ziara ambayo ilifanyika katika mikoa mitano, ambapo wasanii walipiga shoo mbele za mashabiki wao kwa lengo la kuwashukuru kwa ajili ya kuwapigia kura.
Mikoa ambayo ilipata bahati ya kupitiwa na ziara hiyo iliyokuwa imepewa jina la Winner’s Tour, ilikuwa ni Dodoma, Mwanza, Mbeya, Moshi na Mtwara kabla ya juzi kuhitimisha kwenye Viwanja vya Chuo cha Posta.
Pamoja na wasanii kutoa burudani kwenye Winner’s Tour, pia kulikuwa na shindano la kusaka vipaji vya muziki lililoitwa Kili Star Search, ambapo kila mkoa alipatika chipukizi mmoja, ambao kila mmoja alipanda kwenye onesho hilo.
Wasanii waliopanda jukwaani na kukonga nyoyo za mashabiki ni pamoja na Kundi la Raggae, Warriors From the East, African Stars ‘Twanga Pepeta’ washindi wa tuzo ya wimbo bora wa Kiswahili wa bendi, walipanda stejini na kukamua nyimbo tatu ikiwemo wimbo uliowapa tuzo wa Dunia Daraja na kibao chao kipya cha Shamba la Twanga.Wengine ni Kalidjo Kitokololo, Isha ‘Mashauzi’ Ramadhani,
Diamond, Roma Mkatoliki,AT, Ben Pol, Queen Darleen, Suma Lee, Barnaba, Ommy Dimpoz na Ally Kiba.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.