Linapokuja suala la Prezzo kuiwakilisha Kenya katika Big Brother Africa Stargame hata watani wake wa jadi wanampa “tano”.Jaguar adui namba moja wa Prezzo ameapa kumsupport Prezzo kama mwakilishi wa Kenya katika jumba la “Kaka Mkubwa”.Kulikuwepo na wasiwasi kuwa huenda Jaguar angeinyofoa decoder ya DSTV kwa siku 91 ili asishawishe kuwasha TV na kumuangalia Prezzo akiuza sura mjengoni.Lakini Jaguar amezikanusha doubts hizo kwa kudai kuwa hatimaye sasa Prezzo ameenda kufanya kile kinachomfaa na sio muziki kwakuwa hauwezi."Hatimaye Prezzo amepata kitu kinachomfaa. Ni ukweli uliowazi kuwa hawezi kuimba. Yeye ni mwanamitindo na muigizaji hivyo tumwache ajaribu hili na mwisho atengeneze hela yake mwenyewe ambazo atakuwa anajiamini kujisifia” alisema Jaguar.
Hii si mara ya kwanza Jaguar kumsifia Prezzo. Baada ya Prezzo kurudi tena kwenye game mwaka jana, Jaguar alisema amependa muonekano wake mpya kwa kusema ameonesha kukua na anaamini ataendelea kuwa hivyo.Kwa upande wa Prezzo siku zote humponda Jaguar kwa kusema kuwa anachojua ni kwamba Jaguar ni gari. “Simjui Jaguar”. Waambie CMC (wauzaji wa magari ya Jaguar ) kuwa nitakuja kuzijaribu siku moja. Kama nikiipenda basi ntainunua” Prezzo aliwahi kusema.Kwakuwa sasa Prezzo ana uhakika wa kupata shavu la kizushi kutoka kwa Jaguar, huenda mambo yake yakawa mazuri BBA7 na akizikamata $300,000 patakuwa hapatoshi Nairobi!