Mwanamuziki nguli wa miondoko ya Taarab nchini, Khadija Kopa akiimba moja ya nyimbo zake mpya wakati wa tamasha la washindi wa tuzo za Kili Music lililofanyika juzi viwanja vya Chuo cha Posta, Dar es Salaam.
FM Academia
Wanenguaji wa Bendi ya FM Academia (Wazee wa Ngwasuma), kutoka kushoto ni Queen Suzy, Levi Boy, Amina Maradona na Lokolee wakimsapoti rapa bora wa bendi hiyo, Kalidjo Kitokololo (hayupo pichani) kutoa burudani wakati wa tamasha la washindi wa tuzo za Kili Music lililofanyika juzi viwanja vya Chuo cha Posta, Dar es Salaam.
Luiza Mbutu
Kiongozi wa Bendi ya muziki wa Dansi ya African Stars (Twanga Pepeta), Luiza Mbutu akiimba na kucheza wakati wa tamasha la washindi wa tuzo za Kili Music lililofanyika juzi viwanja vya Chuo cha Posta, Dar es Salaam.