Unapozungumzia Wasanii wenye matukio na visa katika tasnia ya filamu jina la Wema Sepetu si geni kwa kila mdau na mpenda sanaa kwa ujumla wake msanii huyu nyota yake ilianza kung’ara mwaka 2006 pale alipochaguliwa kama Miss Tanzania, hivi sasa mwanadada huyo amezidi kung’ara zaidi Utafiti uliofanywa na unaonyesha kuwa kila mtu au msanii aliyewahi kuwa karibu na mwanadada huyo alifanikiwa kwa kujulikana au nyota yake naye kuwa juu kwa kupitia Wema, pia inaonyesha kuwa msanii kama Mr. Blue alipotangazwa kama anatoka na Wema alifanya vizuri sana katika muziki wake.Kuna watu kama Jumbe Yusuf hakuna mtu aliyewajua lakini baada ya kuwepo na Wema ghafla Jumbe alikuwa nyota,utafiti unaonyesha kama utakuwa na uhusiano na msanii huyu na kutangazwa basi nyota yako lazima ipae juu na kuwa gumzo.Mtu mmoja anasema kuwa hata mafanikio ya msanii kama Jb yametokana nay eye kumpa nafasi ya kuigiza katika filamu ya 14 Days ambayo Wema aliigiza kama mke wa JB toka hapo Jb akamudu kumiliki kampuni yake na kuwafunika nyota walikuwa wakitamba awali, kwa sasa JB ndio msanii anayefanya vizuri sokoni katika soko la Filamu..
Msanii kama Charz Baba naye aliwahi kwa na mahusiano na Wema naye ni moja kati ya wasanii waliong’arishwa na nyota ya Wema akiwa bendi ya Twanga pepeta nyota yake kuwa juu na sasa ni Presidaa wa Mashujaa bendi, pamoja na kuandamwa na matukio katika vyombo vya habari ya kashfa bado inaaminika nyota ya msanii uwabeba watu.
Usisahau kuwa msanii huyu pia baada ya kuwa na wasanii fulani mafanikio yao uonekana haraka ila pia umaarufu wa ajabu utokea hivi karibuni kijana aliyetumia nyota ya msanii huyu vizuri na kutokelea mbali Diamond Platnum siku za karibuni aliarikwa kufanya onyesho Big Brother Afrika. Nafasi ya kama hiyo ya umaarufu iliwahi kumtokea msanii nyota marehemu Steven Kanumba ambaye naye aliwahi kuarikwa katika jumba hilo kama mtu maarufu kutoka tasnia ya filamu Tanzania. ...
Wema Superstar kama binadamu ana mapungufu yake lakini ukweli lazima tuseme kuwa mwanadada huyo ni mkali kwa kuwarusha juu wanaokuwa naye karibu kuna mengi yanayomhusu msanii huyu mwenye stori zenye mvuto kwa wanahabari, pengine sisi tunaweza kusema ni shujaa wa habari katika wasanii wa filamu