Filamu ya Chungu iliyorekodiwa katika Jiji la Tanga sehemu za Bumbuli imeibuka filamu bora katika tamasha la filamu Nchi za Majahazi Zanzibar International Film Festival (ZIFF).. akiongea mtayarishaji wa filamu hiyo ya Chungu Dr. Vincensia Shule amesema kuwa ni faraja kwake na wadau wote wa filamu kwa kazi yao kuingia katika tamasha hilo na kushinda tuzo mbili. inatuhamasisha kuendelea kutengeneza filamu zenye ubora zaidi huku tukizingatia mandhari zetu nzuri ambazo hazijatumika na kutangaza utamaduni wetu kwa kiwango cha juu, ushindi huu ni kwa ajili ya wadau wote wa filamu hapa Tanzania, pia ni kichocheo cha watayarishaji wengine kutengeneza filamu zinazotutambulisha sisi ni akina nani,Pamoja na filamu ya Chungu kuibuka kama filamu bora pia mwigizaji mkuu katika filamu hiyo Richard Mshanga ‘Masinde’ ndio mwigizaji bora katika tuzo za ZIFF 2012, Masinde ni mojakati ya waigizaji mahiri katika tasnia ya filamu Nchini, msanii huyo ndiye alikuwa kinara aliyelibeba kundi la sanaa Shirikisho lilokuwa likirusha maigizo yake katika kituo cha Televisheni cha ITV...
KWA HISANI YA FC








