Tuzo nyingine zilizokuwa zikiwaniwa katika tamasha hilo ni zile zilizotolewa na wadhamini wa tamasha hilo Zuku Award ambazo ni filamu bora ya Afrika ambapo filamu ya Inside Stori ya Afrika Kusini ilishinda na muigizaji bora wa Afrika iliyochukuliwa na Kelvin Ndege kutoka kwenye filamu hiyo.Tuzo ya muigizaji bora wa kike Afrika ilikwenda kwa Thuli Khulamelo, Nomfundo Dunazana na Reona Ngiba wote kutoka Afrika Kusini kupitia filamu ya Uhlanga na kuufanya usiku huo kuwa nchi ya Afrika ya kusini.Kwa upande wa tuzo zilizotolewa na ZIFF zilikuwa ni filamu bora fupi iliyokwenda kwa Moccasing ya Kenya, Besti Documentary iliyokwenda kwa marehemu Miriam Makeba kupitia filamu ya Mama Afrika kutoka Afrika Kusini na Best Animation iliyokwenda kwenye filamu ya Ostora ya nchini Syria.
Pia zilikuwepo tuzo ya best Feature Film iliyokwenda kwa filamu ya Uhlanga, Zamora ya Tanzania na muigizaji bora wa Tanzania ikienda kwa Richard Mshanga.Mbali na tuzo za ZIFF, pia kulitolewa tuzo mbalimbali za kimataifa ambapo tuzo ya Ousumane Sembene ilikwenda kwa filamu ya Uhlanga, tuzo ya Signis pia ilikwenda kwa Uhlanga na tuzo ya Verona ikienda pia kwa Uhlanga filamu ya Afrika Kusini.Kwa upande wa tuzo za heshima zilizotolewa na ZIFF, zilikwenda kwa Prof: Martin Mhando na Fabrizio Colombo.
Msimu huu ni wa 15 tangu kuanzishwa kwa tamasha hilo za ZIFF, ambapo awali lilikuwa likijulikana kama tamasha la nchi za Majahazi ambapo tuzo zilianza kutolewa mwaka 1874 na mwaka 1950, zikaanza kutoka rasmi kwa wasanii, jambo ambalo wadau wengi wanajiuliza ni kuwa waandaaji watwasadia vipi watayariashaji wa filamu nchini na kuweza kushiriki vema ikiwa na kuleta ushindani wa kweli katika tamasha hilo?Kwa mfano filamu ya Chungu iliyoshinda tuzo hiyo mtayarishaji wa filamu hiyo yeye aliipeleka kwa ajili ya kuionyesha au tuseme kuizindua baada ya filamu yake kukosa kupokelewa na wasambazaji eti kwa kigezo cha washiriki walioigiza filamu hiyo hawana majina katika soko la filamu, leo hii imetutoa kimasomaso na kuchaguliwa kama filamu bora kutoka Tanzania hapo kuna jambo la kujifunza kwa wale ambao wameshikilia soko la filamu na kujikuta wakiua filamu na kuwakatisha tamaa waandaaji wenye vipaji, taaluma ujuzi wa fani hiyo.Lakini pia wakati umefika kwa waandaaji kubadilisha mfumo wa utoaji taarifa na kuwaangalia wasanii wanaotengeneza filamu wa Tanzania kwa kuwaandaa mapema kwa ajili ya kushiriki katika tamasha hilo kama lengo ni kukuza filamu na kukaribisha watengenezaji wa filamu kutoka nje ya nchi kwa kuwashawishi kuja kutengeneza filamu katika mandhari yetu katika kuvutia watalii na si kuwa na muda mfupi kuja Ngome Kongwe kisha kuondoka kwa sababu tamasha, lakini pia yawapasa kuingia gharama kwa ajili ya matumizi ya lugha ya Kiswahili.Kutumia lugha ya Kiswahili katika vipeperushi na vitu vingine ni kujenga taswira kwa Watanzania kuona ni tamasha lao linawahusu wao na si la watu kutoka nje ambao ndio kila siku wamekuwa wakiibuka kama washindi, kwa mwaka huu tamasha halijasikika sana na kuwatia wadau msisimko kwa kujiona naye anastahili kuwepo Zanzibar kwa ajili ya kushiriki na kuangalia filamu mbalimbali kutoka kila sehemu ya Nchi, mwisho nasema Lugha ya Kiswahili kwa sasa ndio siraha yetu katika harakati za sanaa endepo kitatumika vema.