Google PlusRSS FeedEmail

MSONDO - TWANGA KUWASHA MOTO "CHAGA DAY" LEADERS CLUB

Bendi Twanga Pepeta na Msondo Ngoma zinatarajiwa kutumbuiza kwa pamoja katika show ya aina yake kwenye tamasha la siku ya Wachaga, (Chagga Day 2012),siku ya Julai 28, katika viwanja vya Leaders.
Paul Siboka ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya My Way Entertainment, ambao ndio wameandaa Tamasha hilo la aina yake , alisema siku hiyo watu mbalimbali na familia zao watapata nafasi ya kufurahia kwa pamoja kwa kujionea tamaduni mbalimbali za kabila la Wachaga “Siku hiyo ni ya pekee, kwa familia kujifunza mambo ya utamaduni wa kabila hilo la Chaga, na makabila mengine na burudani kutoka kwa bendi hizo za Twanga na Msondo, pamoja na vikundi vingine vya ngoma ya asili ” alisema Siboka.
Aliongeza kwa kusema kutakua na wazee wa mila ambo watazungumzia asili la kabila la wachaga huku vyakula na vinywaji vya asili kutoka mkoa wa Kilimanjaro,vitapatika amevitaja vyakula hivyo ni kama Kiburu, Ndafu, Shiro, Kitawa, Macharari, Ngararimo, Ng’ande, Kisusio, Mtori, na vingine vingi... Aidha, Tamasha la hilo la ‘Chaga Day’, litafuatia tamasha lingine litakalofanyika Mkoa wa Kilimanjaro, Desemba 22 ambalo nbalo litapambwa na sherehe mbalimbali.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging