Wakati nyota yake ndio inazidi kung'aa kila kukicha, mwanamuziki Diamond Platinumz anatarajia kuigiza kama mhusika mkuu kwenye filamu itakayotayarishwa na kampuni ya Selles Business Inc na kusambazwa na Steps Entertainment.Kwa mujibu mtayarishaji wa filamu hiyo Selles Mapunda, ameifanyia kazi filamu hiyo kwa zaidi ya miezi saba na sasa yupo kwenye hatua ya mwisho ya kuikamilisha.Amesema kwenye filamu hiyo ya Diamond atawashangaza watu kama ilivyokuwa kwenye filamu ya Crazy Tenant aliyoigiza msanii Peter Msechu na Wema Sepetu.Ameongeza kuwa mpaka sasa hajaipa jina filamu hiyo japo Diamond alikuwa na wazo la kuiita filamu hiyo ‘Nimpende Nani’ kutokana na wimbo alioufanya wenye jina hilo na kuongeza kuwa anategemea kutangaza jina la movie hiyo hapo baadae.Amedokeza kuwa katika filamu hiyo Diamond ambaye ni mhusika mkuu ataigiza na muigizaji mmoja wapo kati ya Wema Sepetu ama Jokate Mwegelo.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.