WASHIRIKI MWANZA WAWAKESHESHA MAJAJI
Mkoa wa Mwanza umevunja rekodi kwa kujitokeza zaidi ya washiriki 1100 kwenye usaili wa Bongo Star Search ambapo majaji ilibidi waombe washiriki wengine zaidi ya 150 warudi tena ili kufanyiwa usaili huku ikitakiwa wapatikane washiriki watano tu wa kuiwakilisha Mwanza kati ya hao zaidi ya elfu moja huku Mwanza ukiwa ni mkoa ambayo tayari ulishawahi kutoa washindi wawili wa Bongo Star Search








