
Umati wa Wapenzi wa muziki wa Injili walioingia katika uzinduzi wa albamu ya Hakuna jipya ya msanii mchekeshaji Masanja Mkandamizaji katika Uwanja wa Samora Iringa.

Masanja Lucas Mgaya amesema kuwa wamefurahi sana kwani mwito ulikuwa mkubwa japo onyosho lenyewe lilikuwa limeandaliwa kwa muda mfupi lakini watu walijitokeza kwa wingi na kuhudhuria tamasha hilo lilokusanya wakazi kutoka Ipogolo, Kihesa, Kwa semtema, Mkwawa, Ruaha, Kibwabwa, Igangilonga, Wilolesi, Kitanzani na Ilala.“Kazi nzuri naweza sema tumefanikiwa kwa kuweza kuwaleta wapenzi wa muziki wa Injili na kusherekea vizuri, onyesho lilienda vizuri, tumeanza na uzinduzi wa Albamu ya Hakuna Jipya nyumbani kisha tunaelekea Dodoma kwa ajili ya kuhubiri neno la Mungu kwa njia ya muziki wa Injili,”anasema Lucas.Uzinduzi wa albamu ya Hakuna Jipya ulisindikizwa na waimbaji wakali kama Martha Mwaipaja, Masanja akisindikizwa na rafiki yake wa karibu Silas Mbise, katika uwanja wa Samora ulipamba na nyota wa filamu Nchini kutoka Bongo movie club walipagawisha wapenzi wa filamu za kibongo.
KWA HISANI YA FC







