DJ MICHO MTAALAMU WA 'KUGONGA MIONDOKO' YA KWAITO
Dj Micho anaye 'wapagawisha' kila kukicha mashabiki wa muziki Tanzania kwa kuweza 'kuzidondosha' kwaito za kisasa na kusababisha mashabiki kucheza kwa 'step' huku wakienda sambamba na mapigo bila kukosea wala kuvuluga mtindo huo
Dj Micho ambaye ni mmoja wa ma Dj wa Pro-24 wanaotamba pwani ya Afrika Mashariki kwa 'kupagawishwa'mashabiki wa nyanja za muziki kwa kupiga vionjo vyote vya muziki vinavyopatikana Dunia kote
Dj Micho ambaye jina lake kamili ni Paschal Materego ni msomi wa Chuo cha Mipango Dodoma mwenye stashahada ya Mipango ya Maendeleo ambaye ndoto yake ni na mchango mkubwa kwenye jamii kwa kuwa na mipango endelevu ya kuondoa umasiki katika jamii inayomzunguka
Alianza safari yake ya Dj mwaka 2010 mkoani Dodoma katika Club ya NK ingawa hajasomea fani ya muziki lakini aliweza kumudu kupiga vionjo vyote kwa kile achodai kuwa fani ya muziki ipo kwenye damu
Alidumu ndani ya club hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja huku akiendelea na masomo yake kwa kuwa anapenda fani ya muziki aligawa muda wake vyema ili asivuruge muda wa masomo
Mwaka 2011 nyota yake ilinga'ra na kujiunga na kundi la ma Dj wenye lengo la kuwa wa kimataifa Pro-24 Djs ambapo yuko hadi sasa akiendelea kutoa burudani kwa mashabiki wake
Aliamua kujiunga na kundi hili la Pro 24 Dj ili kukuza fani yake kwani katika kundi hilo pia kuna mafunzo yanayotolewa kwa ma Dj ili kukuza na kuongeza ujuzi wa fani hiyo
Baada ya kuingia katika kundi hilo amejikuta amekuwa na uwezo na ubunifu mkubwa tofauti na alipokuwa awali hivyo anaushukuru uongozi mzima wa kundi hilo kwa kumuwezesha kufika hapo alipofika
Anasema kiwango chake kimeongezeka mara mbili hii inasababishwa na changamoto anazopata ndani ya kundi hilo, na ndio vitu ambavyo alikuwa anapenda kufanya kazi kama kundi ili kuweza kudumu katika fani hiyo kwa kufanya vitu vizuri
Anasema mbali na kupiga muziki ndani ya club mbalimbali sasa anauwezo wa kupiga muziki katika vyombo mbalimbali vya habari na kuongezea kuwa anaweza kutambua na kutofautisha aina ya muziki ya kupiga katika mazingira tofauti tofauti
"Pro-24 ni chuo cha kujifunza fani ya muziki kwa ma dj kwani nilivyofika na sasa ni tofauti nimejikuta najua mbinu nyingi za kujiboresha na kuonekana bora zaidi kutofautisha na dj mwingine" anasema Micho
Akizungumzia utofauti wa pro 24 Dj na ma Dj wengine anasema kuwa wao wanafanya mazoezi na kuchambua muziki kabla hawajapanda kwa ajili ya shoo hali hiyo inawajenga kuijua hadhira hivyo kuhakikisha hadhira hiyo inafurahia kile walichokiandaa
Mbali na hilo pia wao wanatumia vifaa vya kisasa ambavyo vinamsababisha dj kuwa na umakini na kumuongezea uwezo wa kuwa katika ngazi ya kimataifa
Anasema kuwa kila dj kwenye kundi hilo anamiliki vifaa vya kupiga muziki hivyo ni rahisi kwao kufanya mazoezi kila wakati na ndio kikubwa kinachowatofautisha na madj wengine kwani wao wanaamini kuwa dj ni ajira hivyo ni lazima uheshimu ajira yako
Dj huyo anapenda kupiga muziki yenye radha tofauti tofauti amebobea katika miondoko ya Kwaito muziki wa asili ya South Afrika pamoja na muziki wa Bongo Fleva
Mbali na hiyo dj huyo anakitu tofauti kinachomtofautisha na mad Dj wengine kwa kuwa anapiga muziki huku na yeye akicheza miondoko ya muziki huo anaoupiga
Alipoulizwa kwa nini anapenda kucheza wakatia anapiga muziki anasema kuwa "ni mzuka ndio unapanda na ninapokuwa ninacheza ndio nazidi kuwaburudisha mashabiki kwa kuchagua muziki unaoendana na mahari hapo na aina ya mashabiki ambao wapo katika mazingira hayo" anasema
Pamoja na hayo Dj Micho ambaye pia anapiga shoo kubwa za wasanii mbalimbali wanaotoka nchi tofauti anasema kuwa hali hiyo inamsababisha kila siku afikilie kitu tofauti yaani kuwa mbunifu
Anasema tangu alipojiunga na kundi hilo amepata mafanikio makubwa mbali na kuongeza ujuzi pia ameweza kujiendeleza kimaisha
Mbali na kuwa Dj pia ni shabiki mzuri wa timu ya Manchesta huku akiwa anapenda sana kula chakula cha aina yeyote kila ilimradi tu kiwe kimepikwa katika mazingira mazuri
Kwa upande wake yeye hatumia kinywaji chenye kileo chochote kile hii inamjenga kuwa makini kwenye kazi zake na kufikilia kila siku nini afanye ili awe bora
Dj Micho anasema kuwa kazi yao inachangamoto kubwa sana hususani kwenye vishawishi vya kujiingiza katika vitendo vya ngona na wanawake tofauti tofauti
Anaelezea kuwa yeye anajitahidi kupambana na changamoto hizo kwa kuwa na mpenzi mmoja ambaye wanaaminiana na wakati mwingine kuwa naye hata sehemu yake ya kazi ili kuzibitisha kuwa yuko salaama na muaminifu kwa mwenza wake