Ni ijumaa nyingine tena ambapo safu yetu hii ya leo inapambwa na mwanamitindo anayeibukia kwenye fani hiyo kwa kasi huku ndoto zake ni kuwa mwanamitindo wa kimataifa katika sekta za mavazi na ubunifu
Zayna Msekwa ndio jina ambalo linamtambulisha mwanamitindo huyo, ambaye pia ni mwanafunzi katika chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam akisoma stashahada ya Afisa Uhusiano
Zayna anasema kuwa alianza safari yake ya uwanamitindo miaka 4 iliyopita kwa kuanzia kupanda jukwa ambalo liko chini ya kampuni ya British Council katika jukwaa la 'Wapo'
Anasema kuwa baada ya muda alijiunga na kampuni nyingine iitwayo 'Dollywood'ambapo alidumu na kampuni hiyo kwa mwaka mmoja na baada ya hapo ndipo alipotuwa kwa mwanamitindo ambaye pia na yeye ni mbunifu
Zayna anasema kuwa hadi alipofikia sasa anamshukuru Kemi ambaye yeye ni mbunifu wa mavazi kwa kumfikisha alipo sasa kuwa mwanamitindo aliye imara na kuamini kile anachokifanya
Anasema kuwa aliyemvutia zaidi kuingia kwenye fani hiyo ni mwanamitindo Mariam Odemba kwa Tanzania na kwa njee ya nchi hakusita kumtaja Tyra Banks ambaye mpaka sasa hao ndio anawaiga na kufwata nyayo zao
"Nilikuwa natamani kuwa kama Maria siku moja kwa kile alichokuwa anakifanya na mpaka sasa naamini anaweza na teyari amejiwekea hazina, kwani unapokuwa kioo cha jamii watu wanasoma mazuri kutoka kwako" anasema
Anasema kuwa matarajio yake ni kuwa mbunifu wa kimataifa ndani na nje ya Tanzania ili aweze kulitangaza jina la nchi yake
Mbali na hayo Zayna anasema anapenda kuonekana tofauti kwa sababu kila kiumbe yupo tofauti na anapenda kubaki kuwa tofauti