DJ NIJO 'KUKAMUA' SAN SIRO LEO
Wasanii wa filamu na wanamuziki mbalimbali nchini leo watajumuika pamoja katika shoo ya muziki itakayoendeshwa na Dj Nijo kutoka nchini Kenya kwa kushirikiana na ma Dj wa Tanzania
Akizungumza Dar es Salaam mara baada ya kutua jijini Dar es Salaam akitokea nchini Uganda alipokuwa akiendesha shoo kama hiyo, Dj Nijo alisema huo ni mpango wa kuzunguka nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki kuungana na ma Dj wa nchi hizo katika kubadilishana burudani
Alisema alikuwa nchini Uganda kwa shoo kama ambayo ataiendesha Tanzania kwa kushirikiana na ma Dj wa hapa nchini kama Dj Mkali, H'Cue, Peter Moe na Dj Celvin
Akizungumzia onesho hilo Dj H'Cue alisema pamoja na mashabiki wa muziki pia watakuwepo na wacheza filamu maarufu nchini kama Jb, Ray na Aunt Ezekiel ambao wataungana na wasanii wengine katika onesho hilo
Alisema shoo hiyo itafanyika katika klabu ya San Siroambayo imepewa jina la usiku wa fleva na kwamba imeandaliwa na kudhaminiwa na kampuni ya ving'amuzi ya Zuku